Neno La Ushindi___01; Mweleze Mungu shida zako, naye atafanya Mlango nawe utamtukuza.
Neno La Ushindi___01; Mweleze Mungu shida zako, naye atafanya Mlango nawe utamtukuza.
Zaburi 50:15 " Ukaniite siku ya Mateso, Nitakuokoa na wewe utanitukuza.
Huu ni wito wa Mungu kwetu pale tunapokuwa tunapitia katika shida, mateso mbalimbali.
Ya kwamba tumuite Yeye (Mungu ) naye atatusikia na kutuokoa_Uponyaji, kufunguliwa amani, furaha n.k.
Mara nyingi tumekuwa tunawaza na kuwazua wakati pale Magumu yanapotukia katika maisha yetu.Tunaanza kuyafikiria sisi kwanza, badala ya Kuyapeleka kwa Mungu kwanza.
Hivi ndiyo njia sahihi ya kuyapokea matatizo katika maisha yetu.TUMUITE BWANA YESU KATIKA MATESO YETU.na Mungu anakwenda kutuokoa
Haijalishi ni mambo makubwa kiasi gani yanayokusumbua , Lakini hili ndiyo ahadi ya Mungu.
1.Hakuna Ambalo Kwa Mungu haliwezekani_
Mambo yote kwake yanawezekana.
Luka 1:37 " kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu"
Yeremi 32:27 "Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?"
2.Omba lolote nawe utapewa.
Mungu anatoa Tamko kwamba tuombe lolote lile tulitakalo na Mungu atafanya.
Mathayo 7:7-8"Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtaona;bisheni nanyi mtafunguliwa ; kwa maana kila aombaye hupokea;naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
Yakobo 1:5 " Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima[ KITU CHOCHOTE_Mateso, shida na adha mbalimbali], na aombe dua kwa Mungu, awapaye watu wote kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa"
Hivyo nikusihi kwamba usipambane wewe mwenyewe, hiyo VITA SI YAKO bali ni YA Bwana.Peleka mbele zake naye atakuokoa.
Wanadamu hawawezi kukusaidia,bali Mungu anao uwezo UWEZO WA KUKUSAIDIA.
Kwa lolote unalolipita, na Kuona kama haliwezekani lakini kwa Mungu linawezekana kabisa.
Mungu ni mwaminifu na mwenye kushinda ahadi_Aliloahidi kupitia Neno lake ni lazima atatimiza.
Usiogope kwa pito unalopitia, Mwambie Mungu, naye atakuokoa na kukuvusha salama kabisa.
Mungu akubariki sana na Upite salama katika pito unalolipitia.Mwamini Mungu, naye atatenda katika maisha yako.
Uwe na wakati mwema.
Mwl.Joshua Golyama.
+255 764 257 495 (Whatsapp).
golyamajoshua@gmail.com
Comments
Post a Comment