USIKATE TAMAA.....
When giving up is the only option that u have...
U feel like you can't make it.
Hi hali ni kawaida kumpata kila mtu ambaye kuna jambo analifanya na anatamani kulikamilisha..
Unaweza kuhisi kukata tamaa wakati ambao safari yako bado ndefu Sana..
Eliya alifika mahali akajilaza akajiombea kufa wakati ambao safari yake ilikuwa bado ndefu..
Unahitaji kufanya kitu kitakachokupa nguvu za kuendelea mbele..malaika alimtokea Eliya akampa mkate na gudulia la maji wakati ambao yeye aliona imetosha anajiombea afe.1falme19:5
Unaweza kusikia kukata tamaa wakati ambao jambo unalofanya lina ulazima kukamilika haijalishi hali uliyo nayo.
Ilifika mahali Yesu anasema roho yake ina huzuni nyingi kiasi cha kufa,...anasema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke ila si kama nitakavyo mimi bali mapenzi yako yatimizwe.
Ni kweli umechoka ila ulichoanza kukifanya lazima ukimalize.
Jitie nguvu...Yesu aliondoka kwenda kuomba mlimani...kwa huzuni aliyokuwa nayo hata kulala alikuwa hawezi ulikuwa ni wakati wake wa kukesha kwenye maombi...aliomba hadi baadhi ya wanafunzi wake wakeshe pamoja naye ila kuna wakati aliwakuta wamelala.
Saa yako ukiwa umechoka hata wale unaotaka wasimame na wewe huenda wasiweze kwa sababu hali unayoisikia ndani wewe wao hawaioni..kinachokufanya wewe ukeshe wao hawakioni.
Giving up was not an option...alichagua option nyingine ya kukesha kwenye maombi.
Kuomba ilikuwa option yake kila aliposikia hali ya kukata tamaa na kuhisi hawezi kukamilisha kusudi lake.
Alikuwa hata akienda anaanguka lakini pamoja na kuanguka alikuwa anaomba...
Ikiwa bado hujakamilisha kusudi lako usiishie njiani.
Hali ya kukata tamaa ni Hali ambayo inaweza kumpata kila mtu...chagua option nyingine ya kufanya na sio kukata tamaa.
Hali hii iliwapata hata watu wakuu wenye nguvu,waliobeba makusudi makubwa ikiwemo Yesu,Eliya,na mtume Paulo.
Paulo anasema kwa sababu ya yale waliyopitia walikata tamaa ya kuishi
Pamoja na kusikia hali hii Petro alimaliza mwendo na imani aliilinda
Kukata tamaa isiwe ni chaguo lako haijalishi huzuni uliyo nayo,haijalishi hali unayopitia,haijalishi umebaki peke yako huoni tena jinsi ya kuendelea.
Huu ni wakati ambao jitihada binafsi haziwezi kukutoa katika hali hii unahitaji msaada wa Mungu
Eliya alipojilaza malaika alimwamsha akamwambia inuka ule maana una safari ndefu
Yesu alipanda mlimani kwenda kukesha..
Huu ni wakati ambao unahitaji kurecharge ...kuoongezewa nguvu ili uweze kuendelea.
Unahitaji msaada wa Mungu this is the best option don quit!!
We are not living for our selves..hatuishi kwa sababu tunataka kuishi..ipo sababu inayotufanya kuishi...kama hujakamilisha kile kinachokufanya uishi bado huna sababu ya kufa...inuka kula kunywa endelea na safari..don give up..
Though you feel like giving up is only an option that you have but in reality that's not only options...Kuna options nyingi ila option ya kukata tamaa ndiyo inakufanya usione options zingine
Kukata tamaa isiwe ni option utakayochagua ...tafuta kuona options zingine za kukufanya upate nguvu za kuendelea!!
Alphoncina Clement
0714607811
Divine Restoration
The essence of Purpose Discovery
Comments
Post a Comment