Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake.

Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake. 1 Petro 5:6-7 " Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Kila mmoja wetu anataka kufika mbali_mafanikio makubwa sana katika maisha yetu. Pengine kwenye huduma , kazinj kwako na maeneo mbalimbali ya maisha yako. Ipo kanuni moja hapa ambayo tunakwenda kujifunza kwa upana wake, na nina Imani inakwenda kukusaidia kwa viwango vikubwa sana. Kanuni hiyo ni KUNYENYEKEA.Maandiko matakatifu yanaeleza kuhusiana na unyenyekevu, Ya kwamba ili mtu aweze Kuinuliwa na Mungu, Kupanda viwango vya huduma ni lazima anyenyekee. Maana Ya unyenyekevu ni kujishusha na kuona si kitu na kumwinua Mungu zaidi na kumpa nafasi ya kwamba anaweza kufanya mambo makubwa. Unaponyenyekea unakuwa na Maana ya kwamba wewe sio kitu na peke yao hauwezi kufanya chochote.....