YOU SHOULD UNDERSTAND THIS PLEASE
(UNATAKIWA KUELEWA NA KUFAHAMU HILI).
Church is hospital, that's why it's not everybody you meet in church you can marry.
Kanisani ni hospitali, na ndo maana si kila mtu unayekutana
naye, unaweza kumuoa/kuolewa naye
Church is hospital and good hospital is known by the amount of
sick people you see in it.
Kanisa ni hospital na hospital nzuri inajulikana au inatambulika
kwa idadi ya wagonjwa unaowaona katika hospitali hiyo.
Huwezi kusema hospitali fulani ni nzuri na ya Kimataifa halafu
ndani yake hamna mgonjwa hata mmoja.
Unapoenda hospital na kukutana wagonjwa wengi, mwingine
anasumbuliwa na mguu, mwingine unamwona anaharisha pale, mwingine anatapika
pale, mwingine yuko mahututi n.k hiyo ni ISHARA ya Kuonyesha kuwa ni Hospital
nzuri na wanafanya kazi.
Kwa maana hiyo hospital nzuri ni ile ambayo ina wagonjwa wengi
ambao wanashughulikiwa.
Na KANISA ZURI NI KAMA HOSPITAL NZURI,
Kanisani tuna WAONGO, WALEVI, WAZINZI , wako wenye hasira kali,
ni hilo ndilo KANISA ZURI wako hapo KUHUDUMIWA MAGONJWA yao na shida mbalimbali
walizo nazo.
Wako ambao WANAKUBALI KUHUDUMIWA na kuna ambao HAWAKO TAYARI
KUHUDUMIWA.
Kwa hiyo si kila unayekutana naye KANISANI, anafaa kuwa MUME
WAKO/MKE WAKO.
(In church we have insane people, we have fraudsters, we have
liars, and cheats, we have angry people, that's is good Church .We are giving
them treatment, some are responding while others are not yet responding.So It's
not everyone you meet in church you can marry).
NINI FUNZO HAPA(TUNAJIFUNZA NINI).
Usidanganyike kwamba kila mtu anayekutana naye [Kanisani]
ukadhani ni mtu sahihi kwako. Wengine wako hapo kwa sababu fulani fulani.
Usianzishe tu mahusiano na dada/kaka aliyeko kanisani(kwa sababu
yuko kanisani) kabla ya kumfahamu vyema kwa undani wake.Nenda kwa Mchungaji
wake akwambie kiundani, unaweza ukawaza kuanzisha Mahusiano kumbe
ameshachumbiwa au kuolewa kabisa.
Jifunze kupokea Ushauri kabla ya kuanzisha mahusiano yoyote
yale.....
Joshua Golyama
+255 764 257 495 (Whatsapp)
Inspired by Kingslev Okonkwo The Author of Book Who Should I
marry.
Comments
Post a Comment