Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake.

 Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake.

1 Petro 5:6-7 " Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Kila mmoja  wetu anataka kufika mbali_mafanikio makubwa sana katika maisha yetu. Pengine kwenye huduma , kazinj kwako na maeneo mbalimbali ya maisha yako.

Ipo kanuni moja hapa ambayo tunakwenda kujifunza kwa upana wake, na nina Imani inakwenda kukusaidia kwa viwango vikubwa sana.

Kanuni hiyo ni KUNYENYEKEA.Maandiko matakatifu yanaeleza kuhusiana na unyenyekevu, Ya kwamba ili mtu aweze  Kuinuliwa na Mungu, Kupanda viwango vya huduma ni lazima anyenyekee.

Maana Ya unyenyekevu ni kujishusha na kuona si kitu na  kumwinua Mungu zaidi na kumpa nafasi ya kwamba anaweza kufanya mambo makubwa.

Unaponyenyekea unakuwa na Maana ya kwamba wewe sio kitu na peke yao hauwezi kufanya chochote..

Kama mtumishi wa Mungu huna budi kumwomba Mungu akupe unyenyekevu, ili usije kabisa Kuchukua Sifa/utukufu wa Mungu. Na Mtu mwenye unyenyekevu ni yulw ambaye anajua nafasi ya Mungu katika kila Jambo ambalo analifanya, au mafanikio aliyoyapata.

Kinyume cha unyenyekevu ni KIBURI , na huja pale ambapo unashindwa kutambua nafasi ya Mungu katika mafanikio yako. Pale ambapo unajifananisha na watu wengine na kujiona wewe kuwa bora sana kuliko wengine.

Kama unataka kupanda Viwango vya Juu sana, Kupata mafanikio makubwa katika kila ukifanyacho huna budi Kunyenyekea.

Bila Unyenyekevu hauwezi kufanikiwa katika jambo lolote lile.

Jifunze Mambo yafuatayo;

1.Mungu hufanya kila jambo kwa makusudi na kwa wakati wake.

“Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho." Mhubiri 3:11

Hivyo usijilinganishe na mtu yeyote_mafanikio yake kwa kuwa Bwana anafanya kila jambo kwa wakati wake.

2.Mungu huwainua wale wanaonyenyekea kwake, Anayejishusha huyo huinuliwa na Bwana.Maana Mungu huwapa Neema Walio wanyenyekevu.

“......lakini huwapa wanyenyekevu neema." 1 Petro 5:5

3.Mungu huwapinga na Kuwachukia wenye Kiburi.Na Mungi huwashusha wale ambao wana kiburi.Soma Biblia Vizuri utagundua kuwa wote walio kuwa na kiburi Mungu aliwaangamiza.

“Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi,lakini huwapa wanyenyekevu Neema' 1 Petro 5:5 .


4. Tafuta, jifunze na omba Mungu akupe moyo wa unyenyekevu ili uweze kuwa salama.


5. Mungu hatakuinua kabisa katika huduma yako kama utakuwa haujafuzu somo la unyenyekevu na kuanza kuliishi na punde tu ukiwa umeinuliwa na ukaanza kuwa na kiburi Mungu atakushusha chini
Watumishi wengi kipindi hiki hawafanyi vizuri sana ni kwa sababu ya kukosa unyenyekevu. Ukikosa unyenyekevu hautaweza kumsikiliza Bwana anaposema na wewe au kukupa maelekezo.

Bila UNYENYEKEVU Kufanikiwa kwako itakuwa ni NDOTO.

Lipa gharama hii ya kujishusha kwa Mungu wako (unyenyekevu) ili Mungu akuinue kwa wakati wake

ACHA KIBURI na kujiona kuwa wewe ni bora kuliko wengine na kwamba wewe unajua sana kuliko Mungu
Siku ya leo hii iwe AGENDA kwako ya Kutafuta na Kuomba Moyo wa UNYENYEKEVU

MUNGU akusaidie uweze kuwa na Moyo wa Unyenyekevu.

Mwl. Joshua Golyama
+255 764 257 495 (Whatsapp)
golyamajoshua@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

Neno La Ushindi___01; Mweleze Mungu shida zako, naye atafanya Mlango nawe utamtukuza.

USIKATE TAMAA.....