
TAFAKARI YA NENO LA MUNGU Bwana Yesu asifiwe Wapendwa; Tafakari ya Neno la Mungu kutoka ISAYA 29. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimejifunza kutoka katika sura hii ya ISAYA 29. JAMBO LA KWANZA Mungu anatoa ole juu ya mambo yafuatayo kutoka kwenye mstari wa 15. “Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?” — Is 29:15 (SUV) a. Wale wanaomficha Bwana Mungu Mipango yao (Plans). Ambao wanafanya mambo peke yao. Hawataki kumuuliza Mungu/ kumweleza Mungu juu ya mipango yao au kupata direction (mwelekeo) wa mipango yao. “Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.” — Mit 16:9 (SUV) Maana yake ni hii; _Pale unapofanya mambo yako mwenyewe (pasipo kumshirikisha Mungu) ni kutaka kuonyesha kwamba/kukataa kwamba Mungu sio Muumbaji. b. Wale wafanyao maovu huku wakidhani ya kwamba Mungu hawaoni kwa yale wayafanyayo. Huko ni kujidanganya sisi wenyewe. Tusidhani kwamba Mun...