TAFAKARI YA NENO LA MUNGU


Bwana Yesu asifiwe Wapendwa;

Tafakari ya Neno la Mungu kutoka ISAYA 29.



Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimejifunza kutoka katika sura hii ya ISAYA 29.

JAMBO LA KWANZA

Mungu anatoa ole juu ya mambo yafuatayo kutoka kwenye mstari wa 15.

“Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?”

— Is 29:15 (SUV)

a. Wale wanaomficha Bwana Mungu Mipango yao (Plans). Ambao wanafanya mambo peke yao. Hawataki kumuuliza Mungu/ kumweleza Mungu juu ya mipango yao au kupata direction (mwelekeo) wa mipango yao.

“Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.”

— Mit 16:9 (SUV)

Maana yake ni hii;

_Pale unapofanya mambo yako mwenyewe (pasipo kumshirikisha Mungu) ni kutaka kuonyesha kwamba/kukataa kwamba Mungu sio Muumbaji.

b. Wale wafanyao maovu huku wakidhani ya kwamba Mungu hawaoni kwa yale wayafanyayo.

Huko ni kujidanganya sisi wenyewe. Tusidhani kwamba Mungu hatuoni, Matendo yetu yako wazi mbele za Mungu wetu.

Mungu anaona Kila Jambo ambalo mwanadamu anafanya hapa duniani.

JAMBO LA PILI

Ahadi ya Mungu kutulinda na kuwapiga Adui zetu.

Is 29 (SUV)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

⁵ Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.

⁶ Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.

⁷ Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.

⁸ Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.

Wako maadui wengi sana juu yetu, Neno la Mungu linatueleza wazi hapa ambao watatuji kila mara na kwa ghafula. (Mstari wa 5)

Mungu anatuambia kuwa maadui zeti wapiganao na Sisi watakuwa kama Ndoto au maono ya usiku.

Kwa maana kwamba Mungu atatulinda nao.

Kila silaha ambayo itapangwa juu yetu haitafanikiwa, Kila mipango mibaya juu yetu haitaweza kutimia.

JAMBO LA TATU

“Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;”

— Is 29:13 (SUV)

Tumaanishe kile ambacho tunakifanya

_Tuishi yake ambayo tunayakiri kwa vinywa vyetu

Tusifanye mambo ili tuonekane mbele za watu.

_Kulifanyia Kazi/kuliishi Neno la Mungu, tusiwasikilize.

“Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.”

— Ez 33:31 (SUV)

_Lakini tunaonywa kwamba upo wakati ambapo tutatamani sana kulisikia Neno la Mungu lakini hatutaweza

“Na hayo yatakapokuwapo (tazama, yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa nabii amekuwapo kati yao.”

— Ez 33:33 (SUV)

MUHIMU: Waabuduo halisi, tunapaswa kumwabudi Mungu katika Roho na Kweli.

Yoh 4 (SUV)

¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

²³ Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

²⁴ Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Mungu awabariki sana.

 Na Mwl. Joshua Golyama

 


Comments

Popular posts from this blog

Neno La Ushindi___01; Mweleze Mungu shida zako, naye atafanya Mlango nawe utamtukuza.

USIKATE TAMAA.....

NAMNA YA KUANZA UPYA