Posts

Showing posts from October, 2022

MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU

Image
  MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU .   Bwana Yesu asifiwe mpendwa!    Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika na kusema "HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU" Nimemshuhudia Mungu akifanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, nimeshuhudia pia watu wengine wakitendewa mambo makubwa na Mungu.     USHUHUDA WANGU.   "Mwanzoni mwa mwaka 2015, nikiwa kidato cha nne pale Luduga Sekondari, nilianza kuuguliwa na mguu.Maumivu ambayo yalianzia chini ya unyayo wa mguu mfano wa kuchomwa na mwiba, hivyo kuanza kuchechemea.   Maumivu hayo yalipandisha hadi kwenye goti na kuufanya mguu wote kuvimba.. Kuanzia kwenye unyayo wa mguu hadi kwenye goti.   Nilipata maumivu makali sana hadi kulia kila wakati, kutokana na maumivu hayo sikuweza kabisa kutembea. Nilipata dawa kutoka duka la dawa muhimu hazikunisaidia, Nikaenda hospitali nikapewa dawa za namna ile ile lakini hazikuwa na msaada wowote kwangu.   Maumivu ya mguu yalitulia hadi namaliz...