MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU

 

MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU.
 
Bwana Yesu asifiwe mpendwa! 
 
Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika na kusema "HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU"
Nimemshuhudia Mungu akifanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, nimeshuhudia pia watu wengine wakitendewa mambo makubwa na Mungu.
 
 

USHUHUDA WANGU.
 
"Mwanzoni mwa mwaka 2015, nikiwa kidato cha nne pale Luduga Sekondari, nilianza kuuguliwa na mguu.Maumivu ambayo yalianzia chini ya unyayo wa mguu mfano wa kuchomwa na mwiba, hivyo kuanza kuchechemea.
 
Maumivu hayo yalipandisha hadi kwenye goti na kuufanya mguu wote kuvimba.. Kuanzia kwenye unyayo wa mguu hadi kwenye goti.
 
Nilipata maumivu makali sana hadi kulia kila wakati, kutokana na maumivu hayo sikuweza kabisa kutembea. Nilipata dawa kutoka duka la dawa muhimu hazikunisaidia, Nikaenda hospitali nikapewa dawa za namna ile ile lakini hazikuwa na msaada wowote kwangu.
 
Maumivu ya mguu yalitulia hadi namaliza kidato cha nne bila kuuguliwa na maumivu ya mguu.
Desemba 2017, nikiwa Kidato cha Sita, Shule ya Sekondari NJOMBE (NJOSS), maumivu ya mguu yalirejea na sasa yalikuwa mguu wa pili na yakianza kwa staili ile ile.
 
Nilikwenda hospitali ya KIBENA pale NJOMBE, nikafanyiwa X-ray kwenye mguu, majibu hayakuonyesha kuwa nina ugonjwa wowote. Niliandikiwa dawa ili nikazitumie na kupewa maagizo ya kurudi baada ya mwezi mmoja.
 
Hakukuwa na mabadiliko yoyote, nikalimizika kuomba ruhusa ili kwenda hospitali ya IKONDA iliyopo MAKETE kwa ajili ya matibabu zaidi. Nilifanyiwa vipimo vya damu, X-ray ya Mguu na Mkono.. Baada ya kupeleka majibu kwa Daktari. Daktari akasema kuwa haoni ugoniwa wowote na pia X-ray haionyeshi chochote ambacho hakiko sawa.
 
Hivyo, akatupa maelekezo ya kuwaona Madaktari wa mifupa. Daktari wa mifupa hawakuona tatizo lolote, licha ya kuwepo kwa maumivu makali sana kwenye mguu. Zaidi walichofanya nikukamua uvimbe ambao ulikuwepo kwenye goti. Uvimbe ambao ulitoa usaha mwingi pamoja na damu nyingi sana kiasi cha kutosha kwenye kisado. Wakanipa dawa za kutumia kisha kuniruhusu kurudi nyumbani. Wakaniagiza kurudi baada ya mwezi mmoja kwa uchunguzi zaidi.
 
Nikarejea shuleni kuendelea na masomo, .. (kumbuka hapo niko mwishoni wa kidato cha sita.. Nikiwa na maandalizi ya kufanya mtihani wa mwisho wa kidato cha sita).Ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko yoyote ambayo niliyapata baada ya kutoka hospitali.
 
Nililazimika kuomba ruhusa tena pale shuleni, ili nirudi hospitali kwa matibabu zaidi. This time, sikutaka hospitali, niliamua kurudi nyumbani kwa muda.
 
Unajua nini kilichotokea? Kaa nami na endelea kunifuatilia hapa!.Baada ya kurudi nyumbani, Baba yangu akatuhimiza mimi na mama twende kwa Mchungaji ili tufanyiwe maombi. (Baba yangu hajaokoka, lakini hutusisitiza sana kumwomba na kumwabudu Mungu).
 
Mimi na mama yangu tukaenda kwa mchungaji na kumweleza tatizo letu.
 
Mchungaji alituambia hekima zifuatazo;
 
1. Kupitia hili, mimi, Mwanangu Joshua na Mama tutakuwa na maombi ya pamoja kumwomba Mungu kuhusu jambo hili.
2. Tutakuwa na maombi ya mfungo wa Siku 3 kavu tukimwita Mungu.
3. Mungu ni mwaminifu atatusikia na kujibu maombi yetu.
 
"HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU"
 
Hivyo tulianza mambo hayo ya mfungo kwa siku tatu (3). Mungu ni mwaminifu sana, kwa sababu siku ya kwanza tu.. Maumivu yalipungua sana. Tulimwomba Mungu na kumwitaji sana katika tatizo lile.
Nakumbuka tulimaliza maombi siku ya jumapili, Jumatatu nilipanda gari na kurudi shuleni nikiwa mzima wa afya kabisa.
 
Kuanzia siku ile, sijawahi kuyasikia MAUMIVU YA MGUU KABISA. Nilimshuhudia sana Mungu kwa kile ambacho alifanya kwangu. Kwa hakika HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU. Alifanya kwangu, anaweza kufanya na kwako pia.
 
MWAMINI LEO, Atakufanyia Kicheko!.Luka 1:37 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.(SUV)

 
Mwl. Joshua Golyama.
+255 764 257 495
Morogoro

Comments

Popular posts from this blog

Neno La Ushindi___01; Mweleze Mungu shida zako, naye atafanya Mlango nawe utamtukuza.

USIKATE TAMAA.....

Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake.