GHARAMA YA KUJILINGANISHA NA WENGINE
GHARAMA YA KUJILINGANISHA NA WENGINE
Don't compare yourself with someone else!!!
....unapoteza kusudi lako
....Unapoteza uwezo wako
....Hautafanya kwa viwango ulivyotakiwa.
....Hautakuwa na matokeo makubwa
....Huwezi kuwa mkuu kwenye eneo lako kwa kuwa photocopy ya mtu mwingine
.....Unapoteza rasilimali zilizoandaliwa kutimiza kusudi lako.
...God's provisions, alizoandaa Mungu kwa ajili yako..God will never fund something else out of his purpose
Mungu huwa hatoi rasilimali bure..huwa anatoa rasilimali kwa ajili ya kukamilisha kusudi lake.
Unaweza kujifunza kwa wengine wanaofanya vizuri ili uwe bora
Huwezi kuwa bora kwa kuiga bali kwa kujifunza...
Kila mtu anao upekee wake unaomfanya yeye awe bora
Ndani yako Kuna upekee wako wa kukufanya bora...kwa kujifunza unaendelea kuchonga ubora unaoutaka.
Jipime wewe kama wewe,jipime wewe kama unafanya inavyotakiwa ..usijipime kwa kujilinganisha na watu.
Jilinganishe wewe ulivyo na wewe unayepaswa kuwa usijilinganishe na watu umeumbwa kwa utofauti na upekee wako,umebeba kusudi tofauti,utendaji wako uko tofauti na wengine..ukianza kujilinganisha unapoteza upekee wako.
Hupaswi kujilinganisha na mtu yeyote kwa sababu huyo anayo assignment tofauti na yako,anao upekee wake, amepewa kufanya kazi kwa utofauti na wewe.
2 Kor 10:12-18
Huyu ni Petro anaeleza vile anavyojipima yeye kama yeye bila kujilinganisha na wengine usijisifu kwa vipimo vingine..jipime kwenye kusudi lako ulilopewa kutimiza. usijipime kwa vipimo vya watu wengine...
Kila mtu kapewa assignment yake aikamilishe
usijipime utendaji wako na utendaji wa mtu mwingine,usijipime zaidi ya vile unavyotakiwa wewe...
Kuna mahali Mungu anakutaka wewe ufike,usijipimie kuwa umefika kwa sababu Kuna watu bado hawajafika mahali ulipo wewe au usijipimie kwamba bado hujafikia kwa sababu kuna watu wamekutangulia sana.
Tunajipima sisi na matokeo yale tuliyopaswa kuwa nayo na sio sisi na matokeo ya wengine.
Comments
Post a Comment