Posts

NAMNA YA KUANZA UPYA

Kuanza upya ni jambo zuri ambalo linawezekana katika maeneo mengi ya maisha yetu, iwe ni kazi, uhusiano, au malengo binafsi. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua kuanza upya: 1. Tathmini hali ya sasa Anza kwa kufanya tathmini ya hali yako ya sasa.  Jiulize maswali kuhusu maeneo gani unataka kuboresha au kubadilisha. Je, kuna mambo yanayokukwamisha au kukuzuia kufikia malengo yako? Kuelewa hali yako ya sasa ni hatua muhimu katika kuanza upya. 2. Weka malengo Weka malengo wazi na sahihi. Fikiria kwa kina kile unachotaka kufikia na kuamua hatua za kuifikia.  Malengo yako yanapaswa kuwa ya kusisimua, lakini pia yapaswa kuwa ya kufikika na yanayopimika.  Andika malengo yako na uwaeleze kwa uwazi. 3. Panga mpango wa utekelezaji Panga mpango wa vitendo wa jinsi utakavyotekeleza malengo yako. Tambua hatua ndogo na za kivitendo unazoweza kuchukua ili kufikia malengo yako.  Kwa kila hatua, weka muda uliopangwa na rasilimali zinazohitajika. 4. Jifunze kutokana na uzoefu wa...

GHARAMA YA KUJILINGANISHA NA WENGINE

 GHARAMA YA KUJILINGANISHA NA WENGINE   Don't compare yourself with someone else!!! ....unapoteza kusudi lako   ....Unapoteza upekee wako   ....Unapoteza uwezo wako   ....Hautafanya kwa viwango ulivyotakiwa.   ....Hautakuwa na matokeo makubwa   ....Huwezi kuwa mkuu kwenye eneo lako kwa kuwa photocopy ya mtu mwingine   .....Unapoteza rasilimali zilizoandaliwa kutimiza kusudi lako.   ...God's provisions, alizoandaa Mungu kwa ajili yako..God will never fund something else out of his purpose   Mungu huwa hatoi rasilimali bure..huwa anatoa rasilimali kwa ajili ya kukamilisha kusudi lake.   Unaweza kujifunza kwa wengine wanaofanya vizuri ili uwe bora    Huwezi kuwa bora kwa kuiga bali kwa kujifunza...   Kila mtu anao upekee wake unaomfanya yeye awe bora    Ndani yako Kuna upekee wako wa kukufanya bora...kwa kujifunza unaendelea kuchonga ubora unaoutaka.   Jipime wewe kama wewe,jipime wewe kama unafanya inav...

USIKATE TAMAA.....

  When giving up is the only option that u have... U feel like you can't make it.   Hi hali ni kawaida kumpata kila mtu ambaye kuna jambo analifanya na anatamani kulikamilisha.. Unaweza kuhisi kukata tamaa wakati ambao safari yako bado ndefu Sana.. Eliya alifika mahali akajilaza akajiombea kufa wakati ambao safari yake ilikuwa bado ndefu.. Unahitaji kufanya kitu kitakachokupa nguvu za kuendelea mbele..malaika alimtokea Eliya akampa mkate na gudulia la maji wakati ambao yeye aliona imetosha anajiombea afe.1falme19:5 Unaweza kusikia kukata tamaa wakati ambao jambo unalofanya lina ulazima kukamilika haijalishi hali uliyo nayo.   Ilifika mahali Yesu anasema roho yake ina huzuni nyingi kiasi cha kufa,...anasema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke ila si kama nitakavyo mimi bali mapenzi yako yatimizwe. Ni kweli umechoka ila ulichoanza kukifanya lazima ukimalize. Jitie nguvu...Yesu aliondoka kwenda kuomba mlimani...kwa huzuni aliyokuwa nayo hata kulala alikuwa hawezi ulikuwa ni...

MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU

Image
  MGUU KUPONA GHAFLA BAADA YA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU TATU .   Bwana Yesu asifiwe mpendwa!    Ni mara nyingi nimekuwa nikiandika na kusema "HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU" Nimemshuhudia Mungu akifanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, nimeshuhudia pia watu wengine wakitendewa mambo makubwa na Mungu.     USHUHUDA WANGU.   "Mwanzoni mwa mwaka 2015, nikiwa kidato cha nne pale Luduga Sekondari, nilianza kuuguliwa na mguu.Maumivu ambayo yalianzia chini ya unyayo wa mguu mfano wa kuchomwa na mwiba, hivyo kuanza kuchechemea.   Maumivu hayo yalipandisha hadi kwenye goti na kuufanya mguu wote kuvimba.. Kuanzia kwenye unyayo wa mguu hadi kwenye goti.   Nilipata maumivu makali sana hadi kulia kila wakati, kutokana na maumivu hayo sikuweza kabisa kutembea. Nilipata dawa kutoka duka la dawa muhimu hazikunisaidia, Nikaenda hospitali nikapewa dawa za namna ile ile lakini hazikuwa na msaada wowote kwangu.   Maumivu ya mguu yalitulia hadi namaliz...
Image
TAFAKARI YA NENO LA MUNGU Bwana Yesu asifiwe Wapendwa; Tafakari ya Neno la Mungu kutoka ISAYA 29. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo nimejifunza kutoka katika sura hii ya ISAYA 29. JAMBO LA KWANZA Mungu anatoa ole juu ya mambo yafuatayo kutoka kwenye mstari wa 15. “Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?” — Is 29:15 (SUV) a. Wale wanaomficha Bwana Mungu Mipango yao (Plans). Ambao wanafanya mambo peke yao. Hawataki kumuuliza Mungu/ kumweleza Mungu juu ya mipango yao au kupata direction (mwelekeo) wa mipango yao. “Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.” — Mit 16:9 (SUV) Maana yake ni hii; _Pale unapofanya mambo yako mwenyewe (pasipo kumshirikisha Mungu) ni kutaka kuonyesha kwamba/kukataa kwamba Mungu sio Muumbaji. b. Wale wafanyao maovu huku wakidhani ya kwamba Mungu hawaoni kwa yale wayafanyayo. Huko ni kujidanganya sisi wenyewe. Tusidhani kwamba Mun...
Image
  YOU SHOULD UNDERSTAND THIS PLEASE (UNATAKIWA KUELEWA NA KUFAHAMU HILI).                                         Church is hospital, that's why it's not everybody you meet in church you can marry. Kanisani ni hospitali, na ndo maana si kila mtu unayekutana naye, unaweza kumuoa/kuolewa naye Church is hospital and good hospital is known by the amount of sick people you see in it. Kanisa ni hospital na hospital nzuri inajulikana au inatambulika kwa idadi ya wagonjwa unaowaona katika hospitali hiyo. Huwezi kusema hospitali fulani ni nzuri na ya Kimataifa halafu ndani yake hamna mgonjwa hata mmoja. Unapoenda hospital na kukutana wagonjwa wengi, mwingine anasumbuliwa na mguu, mwingine unamwona anaharisha pale, mwingine anatapika pale, mwingine yuko mahututi n.k hiyo ni ISHARA ya Kuonyesha kuwa ni Hospital nzuri na wanafanya kazi. Kwa maana hiyo hospital nzuri ni ile ambayo ina wagonjwa ...

Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake.

Image
 Neno La Ushindi__04; Nyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili akukweze na kukuinua kwa wakati wake. 1 Petro 5:6-7 " Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. Kila mmoja  wetu anataka kufika mbali_mafanikio makubwa sana katika maisha yetu. Pengine kwenye huduma , kazinj kwako na maeneo mbalimbali ya maisha yako. Ipo kanuni moja hapa ambayo tunakwenda kujifunza kwa upana wake, na nina Imani inakwenda kukusaidia kwa viwango vikubwa sana. Kanuni hiyo ni KUNYENYEKEA.Maandiko matakatifu yanaeleza kuhusiana na unyenyekevu, Ya kwamba ili mtu aweze  Kuinuliwa na Mungu, Kupanda viwango vya huduma ni lazima anyenyekee. Maana Ya unyenyekevu ni kujishusha na kuona si kitu na  kumwinua Mungu zaidi na kumpa nafasi ya kwamba anaweza kufanya mambo makubwa. Unaponyenyekea unakuwa na Maana ya kwamba wewe sio kitu na peke yao hauwezi kufanya chochote.....